Alhamisi 24 Aprili 2025 - 21:30
Hawza itambulishwe ulimwenguni kutikana uwezo na sifa zake ilizonazo/ pazuiwe kuchapishwa baadhi ya maudhui za kielimu kabla ya kufanyiwa utafiti

Ayatollah Shabzendeh-dar alisema: Maendeleo na kazi madhubuti ya Hawza, pamoja na fikra za Hawza, bado havijafahamika vya kutosha. Inatupasa kuhakikisha kuwa Hawza inatambulika duniani kwa sifa na ustahiki wake ilionao.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwandishi wa Shirika la Habari la Hawza, Ayatollah Shabzendeh-dar, Katibu wa Shura ya juu ya Hawza, katika kikao na Hujjatul Islam wal-Muslimin Muhammad Baqir Sa’idi Roshan, Mkuu wa taasisi ya utafiti ya Hawza na chuo kikuu, akizungumzia kuhusu baadhi ya taasisi na mashirika ambayo si ya Hawza asilia, lakini yanazidi kuongezeka na kupanuka, alisema: Taasisi hizi mara nyingi hufanya kazi chini ya usimamizi wa mashirika mengine, na kwa namna fulani zimekuwa na upinzani dhidi ya Hawza, iwe kwa upande wa uwezo au utoaji wa vyeti na huenda pia miongoni mwa watu ambao wamekuzwa na kulelewa ndani ya Hawza, taasisi hizi zisiheshimiwe wala kutambuliwa rasmi.

Ayatollah Shabzendeh-dar alisema: Je, Hawza haina uwezo na ustahiki wa kuzirudisha taasisi hizi chini ya mwavuli wa Hawza, ilhali kwa yakini Hawza ina ustahiki huo?

Katibu wa Shura ya juu ya Hawza aliongeza kwa kusema: Maendeleo na kazi ya Hawza pamoja na fikra zake bado havijafahamika. Inatupasa kufanya juhudi ili Hawza itambulishwe duniani kutokana na sifa zake inazostahiki.

Ayatollah Shabzendeh-dar alisisitiza: Ipasavyo kuzuia kuchapishwa kwa baadhi ya maudhui za kielimu kabla ya kuthibitishwa na kusahihishwa. Maudhui hizo ziandaliwe kwa umakini, zikamilishwe na zihakikiwe kwa kina, kisha ziwekwe mbele ya watu wa fikra na uchunguzi, ndipo ziweze kuchapishwa. Kwa sababu hiyo, katika kipindi kilichopita nilipendekeza kwa viongozi wa Hawza kwamba katika Hawza kunahitajika vyumba vya tafakuri (think tanks) ambavyo daima vitakuwa vikishughulikia mada mbalimbali na kuzalisha maudhui.

Mwanzoni mwa kikao hiki, Hujjatul Islam wal-Muslimin Sa’idi Roshan alitoa ripoti kuhusu shughuli na utendaji wa taasisi ya utafiti ya Hawza na Chuo Kikuu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha